
Klabu ya Santos FC imetangaza kumsajili nyota wake wa zamani wa klabu hiyo, Neymar Jr kwa mkataba wa miezi 6 utakaofika tamati mwishoni mwa msimu huu akitokea Al Hilal ya Saudi Arabia
Mbrazil huyo mwenye umri wa miaka 32 anarejea tena katika klabu yake ya utotoni inayoshiriki ligi kuu ya Brazil baada ya kuondoka kwa miaka 12.
Neymar aliichezea Santos Sc mechi 225 na kufunga magoli 136 n kutoa assists 64 kabla ya kutimkia Ulaya kujiunga na FC Barcelona.
Neymar alijiunga na klabu ya Barcelona mwaka 2013 ambapo dunia ilimtambua na kuwa moja ya wachezaji bora sana kabla ya kutimkia PSG mwaka 2017 na kisha kujiunga na Al Hilal mwaka 2023.