
Aliyekuwa mke wa Dr. Ofweneke msanii Niccah the Queen amejitokeza hadharani na kumkingia kifua nyota wa muziki nchini Willy Paul baada ya Diana Marua kudai kwamba Bosi huyo Saldido alijaribu kumbaka.
Kupitia instagram live mrembo huyo amesikitisha na hatua ya Diana Marua kudanganya kuwa alibakwa na Willy Paul ikizingatiwa kuwa kipindi hicho wawili hao walikuwa wapenzi.
Niccah ambaye alikuwa anaishi katika mjengo wa kifahari wa Great Wall Apartment akiwa bado yupo kwenye ndoa na Dr. Ofweneke ameeleza kuwa alikuwa kwenye eneo la tukio wakati Diana alikuwa ndani ya gari ya Willy Paul huku akiwa amekaa bila uwoga wowote.
Hata hivyo amemtaka Diana Marua amwambie mume wake Bahati ukweli badala ya kumbambikia Willy Paul tuhuma za uongo ambazo kwa mujibu wake huenda ikamsababishia msanii huyo tatizo la afya ya akili.