
Zoezi la ugawaji wa tuzo za muziki za AFRIMA (All Africa Music Awards) kwa mwaka 2021 limehitimishwa usiku wa kuamkia leo nchini Nigeria katika Hoteli ya Eko.
Mastaa kadhaa wameweza kujishindia tuzo hiyo kubwa ya muziki kama vile Wizkid, Eddy Kenzo, Fally Ipupa, Mr Flavour na wengineo.
Kenya tumetoka kimasomaso kwenye hafla ya tuzo hizo kupitia Nikita Kering ambaye ameshinda katika kipengele cha “Best Female Artist East Africa” na “Best Artist RnB & Soul.”
Nikita Kering amewashinda wakali kama Rema Namakula, Nandy, Spice Diana, Zuchu, Rosa Ree,Xeniah Manaseh,Karun pamoja na Merry Zerabruk.
Sauti Sol wameibuka washindi kupitia kipingele cha Best group huku msanii chipukizi nchini Shanah Manjeru akishinda kipengele cha Best African Female Artiste
Tuzo za Afrima ambazo zilianza kutolewa tangu mwaka 2015, wawakilishi wengine kutoka Kenya waliokuwa wanawania mwaka huu ni pamoja na Nviiri the story teller, Sauti sol, Nadia Mukami, Khaligraph jones, Tanasha donna, Otile Brown, Xeniah Manaseh, na Muthoni the drummer Queen