Entertainment

Nviiri the Storyteller Akataa Smartphone kwa Ajili ya Kulinda Afya Ya Akili

Nviiri the Storyteller Akataa Smartphone kwa Ajili ya Kulinda Afya Ya Akili

Mwanamuzik Nviiri the Storyteller amefichua kuwa ameachana kabisa na matumizi ya simu aina ya smartphone ili kujiepusha na usumbufu wa mtandaoni na kulinda utulivu wake wa kiakili.

Akizungumza katika Iko Nini Podcast, Nviiri amesema kuwa matumizi ya simu janja yalikuwa yanamchosha kiakili kutokana na presha za mitandao ya kijamii. Amesema tangu aanze kutumia simu ya kawaida, imemsaidia kupata amani, umakini, na nafasi ya kuishi bila shinikizo za mtandao.

Sanjari na hilo, amefichua kuwa ameondoka kabisa jijini Nairobi na kuhamia Limuru, eneo analolitaja kuwa na utulivu, hewa safi na mazingira yanayompa nafasi ya kutafakari na kujipanga upya bila kelele.

Msanii huyo wa Sol Generation, amesema kuwa kuhama kumempa nafasi ya kuzingatia sanaa yake, afya yake ya kiakili, na utamaduni wa maisha yasiyo na haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *