Msanii wa muziki wa hip hop kutoka Kenya, Octopizzo, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea kiti cha ubunge wa eneo la Kibra katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.
Octopizzo, ambaye alizaliwa na kukulia Kibra, amesema anataka kutumia nafasi hiyo kuimarisha maendeleo ya jamii alikotoka, hasa katika sekta za elimu, ajira kwa vijana, na makazi bora kwa wakazi wa mitaa ya mabanda.
Rapa huyo amesema kampeni yake itajikita katika uongozi unaoujali maskini, uwazi, na maendeleo yanayoendana na mahitaji ya wananchi wa kawaida.
Octopizzo anajiunga na orodha ya wasanii nchini Kenya ambao katika siku za hivi karibuni wametia nia ya kuingia kwenye ulingo wa siasa wakilenga kutumia ushawishi wao kuleta mabadiliko chanya katika jamii.