
Kocha wa klabu ya Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anatarajiwa kuendelea kuifundisha klabu hiyo licha ya tetesi za kutimuliwa kushamiri huku Antonio Conte akihusishwa kumrithi.
Haya yote yanajiri baada ya kipigo walichokipokea Man Utd juzi Jumapili kutoka kwa Liverpool cha mabao 5-0, dimbani Old Trafford.
Ripoti mpya kutoka Sky Sports, inaelezwa kuwa, Uongozi unatarajia kujikita zaidi katika kuboresha hali iliyopo kuliko kumtimua kocha Ole Gunnar Solskjaer.