
Bosi wa lebo ya muziki ya White House Music Entertainment Emmanuel Suna maarufu kama Os Suna amefunguka sababu za kubadilisha dini kutoka ukristo kwenda uislam.
Akiwa kwenye moja ya interview Suna amesema alipata wito wa kubadili dini kutoka kwa mwenyezi mungu na hakuna jinsi hangezuia jambo hilo kufanyika.
Hitmaker huyo wa Siri Gambler amekanusha madai yanayotembea kwenye mitandao ya kijamii kuwa alibadili dini na kuwa muislamu kwa sababu alilazimishwa na mwanamke aliyetaka kumuoa kipindi hicho.
Suna amesema wakati aliacha dini ya ukristo alirudi kwa wana familia wake na kuwaomba msamaha kwa hatua ya kubadili dini bila ya kuwataarifu.
Hata hivyo amejinadi kwa kusema kwamba kipindi anakumbatia dini ya kiislam alikuwa na mafanikio makubwa kimuziki kwani nyimbo zake zilifanya vizuri kwenye chati mbali mbali nchini uganda.