Entertainment

PALLASO ADAI HATAKI KUSIKIA HABARI YA NDOA

PALLASO ADAI HATAKI KUSIKIA HABARI YA NDOA

Usitegemee kumuona Pallaso akiingia kwenye ndoa mapema kwa sababu anaona atamuumiza mwanamke.

Pallaso ambaye ni mshindi wa tuzo ya Zzzina Awards amekiri kuwa mpaka sasa ameshakuwa na wanawake zaidi ya 10 lakini hajaona hata mmoja wa kumuoa.

Akipiga stori na Galaxy FM amefunguka kuwa hataki kusikia habari ya ndoa kwani ameelekeza nguvu zake zote kwenye muziki wake.

Hata hivyo Pallaso, amesisitiza kuwa ana watoto na amekuwa akiwalea kama baba anayewajibika.

Ikumbukwe juzi kati Pallaso alidaiwa kuwa amekuwa akichumbiana na msanii mwenzake, Sasha Brighton.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *