Gossip

PENZI LA MULAMWAH NA BABY MAMA WAKE CAROL SONNIE LIMEFIKIA KIKOMO.

PENZI LA MULAMWAH NA BABY MAMA WAKE CAROL SONNIE LIMEFIKIA KIKOMO.

Mpenzi wa siku nyingi  wa mchekeshaji Mulamwah Carol Sonnie ametangaza kuachana na mchekeshaji huyo baada ya kupata mtoto Miezi miwili iliyopita.

Kupitia ukurasa wake wa instagram  Carol Sonnie amesema amechukua maamuzi ya kuachana na mpenzi wake huyo baada ya kuafikia makubaliano ya pamoja ambapo amedai kuwa wataendelea kuwa marafiki huku wakimlea mtoto wao kama wazazi wenza.

Hata hivyo chanzo cha wawili hao kuachana hajaweka wazi ila sio mara ya kwanza kufanya hivyo kwani kipindi cha nyuma wamekuwa na mazoea ya kuachana na kisha mwisho wa siku wanarudiana.

Baada ya mrembo kuthibitisha taarifa za kuachana kwao mchekeshaji Mulamwah alienda mbali zaidi na kumtambulisha mpenzi wake mpya aitwaye Ruth.

Ikumbukwe Mulamwah ambaye ni baba ya mtoto mmoja kwa sasa na  baby mama wake Carol Sonnie waliweka wazi uhusiano wao mwaka wa 2017.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *