Sports news

Posta Rangers kuivaa Gor Mahia katika pambano la kukata na shoka Nyayo Stadium.

Posta Rangers kuivaa Gor Mahia katika pambano la kukata na shoka Nyayo Stadium.

Ligi Kuu ya Soka nchini Kenya inaendelea kushika kasi, huku macho yote yakielekezwa kwenye mchuano mkali utakaopigwa Jumapili hii kati ya vinara wa ligi, Posta Rangers, na mabingwa wa kihistoria, Gor Mahia.

Rangers, ambao hawajapoteza mechi yoyote msimu huu, wameshinda michezo mitatu na kutoka sare mara moja, na wanaongoza jedwali kwa pointi 11 baada ya raundi nne. Kwa upande mwingine, Gor Mahia walianza msimu kwa kupoteza dhidi ya Bidco United, lakini wakarejea kwa kishindo kwa ushindi dhidi ya Mara Sugar na KCB. Kwa sasa, K’Ogalo wako nafasi ya nne kwa pointi sita.

Posta Rangers wanasaka taji lao la kwanza, ilhali Gor Mahia wanapigania kuongeza taji lao la 22 kwenye historia yao tajika.

Katika michezo mingine ya raundi ya tano: Mara Sugar watapambana na Bidco United Ijumaa hii Oktoba 24 mjini Kericho, Kariobangi Sharks wataialika APS Bomet siku ya Jumamosi, huku AFC Leopards wakiwania ushindi wao wa kwanza dhidi ya KCB.

Jumapili, Shabana itavaana na Mathare United huko Gusii, na Murang’a Seal itamenyana na Tusker mjini Murang’a.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *