
Nyota wa muziki wa Bongofleva Professor Jay ametangaza ujio wa ngoma yake mpya ambayo amemshirikisha G-nako.
Rapa huyo mkongwe wa muziki nchini Tanzania ametuweka wazi hilo kupitia kurasa zake za mitandao ya Kijamii huku picha ikimuonesha akiwa studio na mtayarishaji Bin Laden wa Tongwe Records.
Ni muendelezo wa Kolabo zake na vijana wa sasa kwenye muziki wa bongo fleva, ngoma ambayo ipo masikioni mwetu kwa sasa ‘Shikilia’ amewapa mashavu wakali wa kizazi hiki kama Maua Sama na Young Lunya.
Ni miezi Nane sasa tangu Prof Jay kuanza kushusha mangoma makali, mkwaju wake wa kwanza ulikuwa ‘Utaniambia nini’