Entertainment

PROMOTA ABTEX AZIDI KUMRUSHIA VIJEMBE PALLASO, ADAI TAMAA YA PESA ITAMPONZA KWENYE MUZIKI WAKE

PROMOTA ABTEX AZIDI KUMRUSHIA VIJEMBE PALLASO, ADAI TAMAA YA PESA ITAMPONZA KWENYE MUZIKI WAKE

Promota wa muziki nchini Uganda Abtex Musinguzi hana furaha kabisa na jinsi msanii Pallaso anasimamia shughuli zake za kibiashara.

Kulingana na Abtex ,Pallaso pallaso na uongozi wake wamekuwa na mazoea ya kuchukua shows nyingi jambo ambalo limepelekea msanii huyo kushindwa kutumbuiza kwenye show zote ambazo amepewa.

Promota huyo amemtaka Pallaso pamoja na uongozi wake aache tamaa ya pesa la sivyo wao kama mapromota watachukua maamuzi magumu ya kumaliza career ya Pallaso kwa kutompea michongo ya shows kwani msanii huyo anawavunjia mashabiki heshima kwa kususia shows.

Utakumbuka juzi kati Pallaso alilazimika kufagia mji wa masaka kama njia ya kuwaomba mashabiki zake msamaha baada ya kuchelewa kufika kwenye perform yake  siku Wapendanao Duniani.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *