
Rapper kutoka nchini Marekani, Kodak black ameingia kwenye headlines na kuzua mijadala kwenye mitandao ya kijamii baada ya kusambaa kwa video clip inayo muonesha akicheza na mama yake katika mtindo usiopendeza.
Katika video hiyo Kodak anaoneka akicheza na mama yake mzazi, kwenye sherehe ya Birthday yake huku akimshika mama yake mzazi makalio (yaani kama anacheza na demu wake hivi) na kuendelea kufanya ujinga mwingi kwa kutaka pia kumkiss mdomoni.
Kitendo hiki kimeibua mijadala na kuteka hisia za watu mbalimbali duniani, wengine wakidai Kodak amefanya udhalilishaji wa kijinsia kwa mama yake mzazi.