
Rapa Offset anatamani angepata nafasi moja tu ya kutumbuiza na TakeOff kabla ya Mungu hamjachukua, lakini nafasi moja ya mwisho kucheka pamoja. Maneno haya yameandikwa kwenye barua ya Offset kwenda kwa marehemu Take Off ambaye alifariki dunia November Mosi kwa kupigwa risasi.
Offset ameandika “Maumivu ambayo umeniachia hayavumiliki. Moyo wangu umevunjika na nina vitu vingi sana vya kusema lakini nakosa maneno. Nimekuwa nikienda kulala na kuamka nikitumai kwamba yote haya ni ndoto tu. Lakini ni uhalisia, na uhalisia nauhisi kama ni njozi tu. Kila mara uliponiona, hukunipa salamu ya mkono, ulinipa kumbato.”
“Natamani ningekukumbatia kwa mara ya mwisho. Tuvute wote kwa mara mwisho. Tutumbuize kwa mara ya mwisho. Nafahamu mtu mwenye roho kama yako yupo peponi kwa sasa. Natumai unajionea jinsi gani tunakupenda na kukukumbuka. Umeacha shimo kwenye moyo wangu ambalo haliwezi kuzibwa. Nitakupenda daima.”