
Rapa kutoka marekani T.I, ametema cheche za maneno kwamba hakuna anayemuweza kwenye muziki kuanzia Jay-Z, Kanye West, Nas na Lil Wayne.
Kupitia insta story yake, mkali huyo ameweka video inayomuonesha akisema waleteni hao wakali wenu na kuwataja majina akisema hawamuwezi kwa lolote kwenye muziki.
“Unapozungumzia kuhusu kufanya muziki, unapozungumzia kuhusu kuweka rekodi, kuachia ngoma kali, hakuna yeyote anayeniweza.”
Rapa huyo kutoka Atalanta amesema kuna rappers wanakataa kufanya naye kazi kwa sababu wanaogopa atawafunika; “Jay-Z na Nas inabidi muwalete, waleteni. Hao si ndio mnawataka. Jay-Z, Nas, Lil Wayne na YE hao ndio mnawataka, waleteni. Pusha T, ndio, wote. Hakuna anayeniweza.” alisema T.I.