Mwanamuziki mkongwe wa Bongo Fleva, Ray C, ameonyesha kutoridhishwa na baadhi ya wasanii wanaoendelea kupromote nyimbo zao kwenye mitandao ya kijamii wakati taifa likiwa katika kipindi cha huzuni na maombolezo kufuatia ghasia za baada ya uchaguzi.
Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Ray C amehoji dhamira ya wasanii wanaoendelea kufanya kampeni na challenge za nyimbo zao katika kipindi ambacho Watanzania wengi wanalia na kuomboleza vifo vya wapendwa wao.
Hitmaker huyo wa Wanifuatia Nini, amesema kuwa ni muhimu kwa watu wa tasnia ya muziki kuonyesha utu na kusimama pamoja na wananchi wakati wa majonzi badala ya kuendelea na shughuli za burudani kana kwamba hakuna kilichotokea.