Entertainment

Rayvanny atuhumiwa kushindwa kumlipa prodyuza

Rayvanny atuhumiwa kushindwa kumlipa prodyuza

Baada ya Mwanamuziki Rayvanny kutoka hadharani na kudai kwamba aliilipa Label ya WCB kiasi cha KSh. Million 53 na kuvunja mkataba wake, Mtayarishaji wa Muziki nchini Tanzania Zest ameibuka na madai yakejuu ya msanii huyo.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mtayarishaji huyo ambaye aliwahi kuzipika ngoma kadhaa za Rayvanny amesema Bosi huyo wa Next Level Music ameshindwa kumlipa hata Elfu 2 za KenyaΒ yaΒ kazi zote ambazo amewahi kumfanyia.Aidha ametoa angalizo kwa maprodyuza kuacha kuwasindikiza wasanii kwenye utajiri ilhali wanaisha maisha ya umasikini mtaani.

“Dogo kalipa 1.3 Bilion kuondoka Wasafi lakini anashindwa kunilipa ata elfu 50 ya kazi zote nilizowahi kumrecord, kuna namna Producers tunatakiwa kujitazama tunasindikiza sana watu kwenye utajiri.”

“Sasa naona ni muda sahihi wa kufwatilia haki zangu zote 2023 nataka malipo ya ngoma zote nilizowahi kutengeneza maana mpaka sasa pesa zinaingia kupitia kazi nilizowahi kuzifanya na sioni kitu”. ameeleza Zest kwenye ujumbe wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *