Entertainment

Rayvanny Awataka Watanzania Kudumisha Amani

Rayvanny Awataka Watanzania Kudumisha Amani

Msanii nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Rayvanny, ameungana na Watanzania katika kuomboleza vifo vya watu waliopoteza maisha kufuatia ghasia zilizoripotiwa baada ya uchaguzi wa Oktoba 29.

Kupitia ujumbe aliouchapisha mtandaoni, Rayvanny amesisitiza umuhimu wa Watanzania kuendelea kushikamana kwa umoja na upendo, akisema sifa kuu ya taifa hilo tangu enzi za mababu imekuwa ni amani na mshikamano.

Hitmaker huyo wa Tetema, ameeleza kuwa ni muhimu kulinda na kutunza zawadi ya amani ambayo Mungu amewapa Watanzania, huku akitoa pole kwa familia, ndugu, na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika matukio hayo ya huzuni.

Rayvanny aamehitimisha ujumbe wake kwa kuwataka wananchi waendelee kuishi kwa upendo na amani, akisisitiza ujumbe wa “Sisi ni ndugu” kama njia ya kuhimiza umoja wa kitaifa katika kipindi hiki kigumu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *