
Sasa unatakiwa kutanguliza neno ‘Mheshimiwa’ pale unapolitaja jina la Rihanna, Novemba 30 mwaka huu msanii huyo ametunukiwa cheo cha heshima kwa kutangazwa kuwa Shujaa wa taifa la Barbados.
Rihanna ametunukiwa wadhifa huo na Waziri Mkuu wa taifa hilo Mia Mottley mbele ya Rais mpya wa nchi hiyo Bi. Sandra Mason kwenye hafla ya taifa la Barbados kuondoka rasmi kwenye utawala wa Malkia Elizabeth wa pili wa Uingereza ambao ulidumu kwa miaka 55.
Rihanna anakuwa shujaa wa 11 katika taifa la Barbados na wa kwanza kutunukiwa tangu mwaka wa 1998.
Riri ambaye amekuwa akipaza sauti kuhusu Barbados na vivutio vyake pia ni balozi wa Utalii katika taifa hilo.