Mshambuliaji wa Senegal, Sadio Mane rasmi ataikosa michuano ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar.
Mane ameondolewa kwenye Kikosi cha Simba wa Teranga baada ya kushindwa kupona kufuatia kupata majeraha kwenye mechi ya Bayern Munich dhidi ya Werder Bremen wiki iliyopita.
Awali Sadio Mane alitajwa na kocha Aliou Cisse kwenye kikosi cha wachezaji 26 wa Senegal kushiriki kwenye fainali ya kombe la dunia, licha ya kuwa na jeraha hilo.
Aidha, fainali za kombe la dunia Qatar zinatarajiwa kuanza Jumapili hii, Novemba 20 na kumalizika Jumapili ya Desemba 18.