Sports news

Serikali Kenya Kushirikiana na Waandalizi wa Nairobi Marathon Kuboresha Utalii wa Michezo

Serikali Kenya Kushirikiana na Waandalizi wa Nairobi Marathon Kuboresha Utalii wa Michezo

Waziri wa Utalii, Bi. Rebecca Miano, amesema serikali iko tayari kushirikiana na waandalizi wa mbio za kila mwaka za Nairobi Standard Chartered Marathon ili kuboresha hadhi ya mashindano hayo na kuyatumia kama nyenzo ya kukuza utalii wa michezo nchini.

Akizungumza leo katika Bustani ya Uhuru, Nairobi, wakati wa makala ya 22 ya mbio hizo, Miano ameeleza kuwa sekta ya utalii na michezo zina uhusiano wa karibu unaoweza kuchochea ukuaji wa uchumi wa taifa.

Amesema serikali inapanga kuanzisha ushirikiano wa kimkakati na washikadau katika sekta ya michezo, utalii na masoko ya kimataifa, ili kuhakikisha Kenya inatambulika duniani kama kitovu cha utalii wa michezo.

Waziri Miano pia amepongeza ufanisi wa waandalizi na washiriki, akibainisha kuwa takribani wanariadha 32,000 walijitokeza kushiriki katika mbio za mwaka huu idadi ambayo inaonyesha mvuto mkubwa wa mashindano hayo kitaifa na kimataifa.

Hata hivyo, amesema wizara yake itaendelea kuunga mkono matukio kama haya yanayochangia ustawi wa michezo, utalii na uchumi wa nchi kwa ujumla

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *