Entertainment

Serikali Yakanusha Utetezi wa Lil Durk Kuhusu Mistari ya Muziki

Serikali Yakanusha Utetezi wa Lil Durk Kuhusu Mistari ya Muziki

Mamlaka za Marekani zimejibu vikali utetezi wa rapa Lil Durk, ambaye anadai kuwa analengwa kwa sababu ya mistari ya nyimbo zake, si kwa makosa ya jinai.

Katika taarifa yao, waendesha mashtaka wameweka wazi kuwa Durk hashtakiwi kwa sababu ya muziki wake, bali kwa madai ya kupanga njama ya mauaji ya kikatili, iliyotokea mwaka 2022 dhidi ya rapa mwenzake Quando Rondo, na kupelekea kifo cha mtu mmoja.

Hii ni baada ya wakili wa Durk kudai kuwa msanii huyo anaonewa na kuwa serikali ina jaribu kuchukulia ubunifu kama uhalifu, kwa kutumia mistari ya nyimbo kama ushahidi wa jinai. Hata hivyo, waendesha mashtaka wamesema kuwa hata baada ya kuondoa mistari ya muziki kutoka kwenye hati mpya ya mashtaka, bado kuna ushahidi wa kutosha kumhusisha Durk na shambulio hilo.

Kwa upande wake, timu ya mawakili wa Durk inaendelea kupambana mahakamani, ikiomba kesi ifutwe na pia kusisitiza apewe dhamana akisubiri kesi yake iliyopangwa kusikizwa Oktoba mwaka huu.

Wakati mashabiki wakisubiri kuona mwelekeo wa kesi hii, gumzo linaendelea kuhusu uhuru wa wasanii kuzungumza kupitia muziki bila kuogopa kufunguliwa mashtaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *