
Mwanamuziki kutoka Uganda Shakira Shakira ameibua gumzo kwa kauli zake zenye utata kuhusu tendo la ndoa, uaminifu wa ndoa na jinsi wanawake wanavyoweza kuwadhibiti wanaume wao kwa njia ya faragha.
Katika mahojiano na YouTuber mmoja nchini humo, Shakira alifichua kuwa njia bora ya kumfanya mwanaume asitoke nje ya ndoa ni kuhakikisha anaridhishwa chumbani. Msanii huyo alieleza kuwa yeye huwa hajizuizi anapokuwa na mumewe, bali huwapa kila aina ya kimapenzi na kumfurahisha kikamilifu.
“Ukilala na mwanaume, hakikisha anatoka akiwa ameridhika kabisa. Mpe kila kitu. Jaribu kila mtindo. Usione haya ukiwa naye. Ukifanya hivyo, atakuona wewe ni dunia yake. Mwanaume aliyeridhika hana sababu ya kutangatanga,” alisema Shakira.
Shakira alidai kuwa wanawake wengi hupoteza waume wao kwa sababu hawawapi utulivu wa kimapenzi, na badala yake hupambana na wanawake wengine kwa wivu na kelele zisizo na msingi. Alishauri wanawake kuwa wabunifu na wazi katika mahusiano yao.
“Usipigane na wanawake wenzako kwa sababu ya mwanaume. Badala yake, chukua jukumu la kuhakikisha mume wako anaridhika. Ukimpa amani chumbani, atakupa amani maisha yote,” aliongeza.
Shakira pia alisisitiza umuhimu wa mawasiliano ya wazi kati ya wapenzi, akisema kuwa uaminifu na uhuru wa kujieleza katika uhusiano ndiyo msingi wa mapenzi ya kudumu.
Kauli hizi zimezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi wakimpongeza kwa kusema ukweli ambao wengi huogopa kuusema, ilhali wengine wakimshutumu kwa kushusha maadili ya jamii.