
Taarifa zinazotembea kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa zinadai kuwa mwanamuziki Sheebah Karungi kutoka Uganda amejiondoa kwenye uongozi wake wa Team No Sleep ambao unasimamiwa na Jeff Kiwa
Sheebah Karungi, aliyekuwa mwanachama wa kundi la The Obsessions, alijiunga na Team No Sleep mwaka wa 2013 na tangu wakati huo ametengeneza jina kupitia muziki wake barani Afrika.
Kwa miaka ambayo amekuwa kwenye muziki, ametoa ngoma kali, ameshinda tuzo nyingi,lakini pia amekuwa mfanyabiashara mkubwa ambaye anaangaliwa na vijana wengi nchini Uganda.
Tetesi mpya zinadai kuwa Sheebah na meneja wake Jeff Kiwa wameingia kwenye ugomvi kutokana na masuala yanayohusiana na pesa.
Kulingana Mwanahabari maarufu nchini Uganda Jenkins Mukasa Team No Sleep inamtafuta msanii mpya atakayechukua nafasi ya Sheebah. Jenkins amesema kwa sasa Sheebah anasimamiwa na mtu aliyekuwa anaratibu shows zake akiwa chini ya Team No Sleep
Hata hivyo Sheebah hajatoa tamko rasmi kuhusu uvumi huo ikizingatiwa kuwa hii si mara ya kwanza kwa msanii huyo kuripotiwa kuachana na Team No Sleep.