Tech news

Snapchat Yaanza Kutoza Watumiaji Kuhifadhi Picha na Video

Snapchat Yaanza Kutoza Watumiaji Kuhifadhi Picha na Video

Snapchat imetangaza kuwa itaanza kuchaji watumiaji wake wanaotumia huduma ya kuhifadhi picha na video ndani ya mtandao huo, maarufu kama Snapchat Memories.

Kupitia tangazo rasmi, kampuni hiyo imesema kuwa watumiaji ambao wamehifadhi picha na video zaidi ya 5GB watatakiwa kulipia ada ili kuendelea kuhifadhi kumbukumbu zao mtandaoni. Huduma hiyo mpya itawapa watumiaji fursa ya kununua nafasi ya ziada ya kuhifadhi hadi 250GB.

Watumiaji wa kawaida watapokea muda wa miezi 12 kuhifadhi na kuhamisha picha zao kutoka Snapchat kwenda kwenye vifaa vyao binafsi ili kuepuka kupoteza data ikiwa hawataki kulipia huduma hiyo.

Hata hivyo, watumiaji wa Snapchat+, huduma ya kulipia ya kampuni hiyo, watakuwa na nafasi ya kuhifadhi hadi 250GB bila malipo ya ziada.

Ada ya kuhifadhi data zaidi itakuwa takriban KSh 4,895 kwa mwezi kwa watumiaji wasiojiunga na Snapchat+.

Mabadiliko haya yanakuja kama sehemu ya mkakati wa Snapchat kuongeza mapato kupitia huduma zake za kidigitali na kutoa nafasi bora zaidi kwa watumiaji wake.

Snapchat haijataja tarehe rasmi ya kuanza kwa mfumo huu, lakini inatarajia kuanza kwa awamu katika maeneo mbalimbali duniani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *