Msanii wa muziki, Stevo Simple Boy, amewasisimua mashabiki wake mitandaoni baada ya kushiriki wishlist yake ya siku ya kuzaliwa iliyojaa vionjo, mizaha na ndoto kubwa za maisha.
Kupitia orodha hiyo, Stevo ameonyesha wazi matamanio yake akigusia masuala ya mapenzi, mafanikio, umaarufu na maisha ya kifahari. Miongoni mwa aliyoyataja ni kutamani kuwa na bibi wa pili mwenye nyash, huku akisisitiza asiwe wa kuuliza password za simu au mitandao ya kijamii.
Katika upande wa teknolojia na mali, Stevo ameomba iPhone 17 ya rangi ya chungwa, pamoja na gari la pili aina ya Toyota Crown. Pia ametaja hitaji la soksi mpya zisizo na mashimo, jambo lililowafanya mashabiki wengi kucheka na kujihisi karibu naye.
Kwa upande wa maisha ya kifedha, Stevo ametamani M-Pesa balance kubwa, awe na pesa kama za Chief Godlove, na hata Wi-Fi ya jirani iache kumkataa. Katika ndoto zake za kimataifa, msanii huyo ametaja safari ya Dubai, akiiandika kwa mtindo wake wa kipekee kama “Dubal.”
Si hayo tu, Stevo Simple Boy pia ametamani nyota na umaarufu kama wa IShowSpeed, pamoja na kupata collabo na Khaligraph Jones, akionyesha nia yake ya kupanua wigo wa muziki wake wa kwenda kimataifa.