Alikiba Amtambulisha Meneja Mpya Kings Music

Alikiba Amtambulisha Meneja Mpya Kings Music

Staa wa muziki wa Bongo Flava na mmiliki wa lebo ya Kings Music Records, Alikiba, ametambulisha rasmi meneja wake mpya, Benjamin Otwal, katika hafla iliyofanyika jana nchini Kenya. Kupitia utambulisho huo, Alikiba amemkaribisha Benjamin Otwal kama sehemu ya uongozi mpya unaolenga kuimarisha shughuli za muziki na biashara za Kings Music ndani na nje ya Afrika Mashariki. Utambulisho wa meneja huyo mpya umechukuliwa kama hatua muhimu katika mkakati wa Alikiba wa kupanua wigo wa kazi zake, kusimamia miradi mikubwa ya muziki na kuongeza ushirikiano wa kimataifa. Hafla hiyo iliyofanyika Nairobi imeonyesha pia dhamira ya Alikiba kuimarisha mahusiano ya kisanaa na kibiashara kati ya Tanzania na Kenya, huku Kings Music Records ikiendelea kujipanga kama moja ya lebo zenye ushawishi mkubwa katika ukanda huu.

Read More
 Alikiba Aibua Taharuki Baada ya Kupost Picha ya Zamani Akiwa na Diamond Platnumz

Alikiba Aibua Taharuki Baada ya Kupost Picha ya Zamani Akiwa na Diamond Platnumz

Staa wa muziki kutoka Tanzania, Alikiba, amezua gumzo kubwa mtandaoni baada ya kupakia picha ya zamani akiwa pamoja na mpinzani wake wa muda mrefu, Diamond Platnumz, kupitia ukurasa wake wa Snapchat. Kitendo hicho kimewasha moto wa mijadala mitandaoni, kwa sababu wawili hao wamekuwa wakitajwa kuwa na uhasama wa muda mrefu ndani ya tasnia ya Bongo Fleva. Mashabiki wengi wameonekana kushangazwa na hatua hiyo, huku wengine wakihisi kwamba huenda tofauti zao tayari zimewekwa pembeni. Picha hiyo imefungua mlango wa tetesi mpya, baadhi ya mashabiki wakijiuliza kama wakati umefika kwa Alikiba na Diamond kufanya collabo ya pamoja, jambo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa hamu kwa miaka mingi. Wadau wa muziki wanasema kitendo hicho ni ishara kwamba huenda upepo mpya unavuma katika tasnia, na inawezekana wawili hao wako kwenye hatua ya kurudisha mahusiano mazuri kikazi.

Read More
 Ali Kiba Aomba Msamaha Watanzania kwa Kujihusisha na Siasa

Ali Kiba Aomba Msamaha Watanzania kwa Kujihusisha na Siasa

Mwanamuziki nyota wa Bongo Fleva Alikiba ameomba radhi kwa Watanzania kufuatia hasira zilizozuka baada ya yeye kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan wakati wa kampeni za uchaguzi wa hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alikiba amewaomba radhi Watanzania kwa kuwaumiza kupitia msimamo wake wa kisiasa na kuwapa pole wale wote waliopoteza maisha au kujeruhiwa wakati wa machafuko yaliyoshuhudiwa baada ya uchaguzi, wakiwa wanaitetea nchi yao. Kauli yake imekuja wakati ambapo wananchi wengi nchini Tanzania wamekuwa wakikosoa baadhi ya wasanii wakubwa nchini humo waliounga mkono serikali ya Rais Samia Suluhu iliyopewa lawama kwa kutumia nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji. Hata hivyo, wafuasi wengi mtandaoni wamesema msamaha huo umechelewa, lakini ni hatua muhimu katika kuponya majeraha ya kijamii yaliyosababishwa na siasa zenye mgawanyiko nchini Tanzania.

Read More