Charisma Afunguka Kuhusu Ulevi Uliomfikisha Kwenye Hatari ya Kujitoa Uhai

Charisma Afunguka Kuhusu Ulevi Uliomfikisha Kwenye Hatari ya Kujitoa Uhai

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Charisma, amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto alizopitia kutokana na matumizi ya pombe kupindukia. Akipiga stori na Iko Nini Podcast, msanii huyo ameeleza kuwa hali hiyo ilimfikisha kwenye msongo wa mawazo mkubwa kiasi cha kufikiria kujiua kwa kujinyonga akitumia kamba. Katika tukio hilo, baba na ndugu yake waliingilia kati na kumuokoa akiwa kwenye jaribu hilo. Charisma amesema kuwa maumivu aliyoyapitia na kuona familia yake ikilia na kuomba kwa ajili yake vilimfanya achague kubadilika. Kwa sasa, msanii huyo ameanza ukurasa mpya wa maisha, akilenga muziki na familia kama nguzo za matumaini na uponyaji. Hata hivyo, ameahidi kutumia jukwaa lake kuelimisha na kuhamasisha vijana dhidi ya matumizi ya pombe kupita kiasi, akisisitiza kuwa pombe si suluhisho bali ni njia ya kuangamiza ndoto na maisha.

Read More
 Charisma Atetea Muziki wa Kenya Baada ya Kauli kuwa Tanzania ni Bora Kimuziki

Charisma Atetea Muziki wa Kenya Baada ya Kauli kuwa Tanzania ni Bora Kimuziki

Msanii anayechipukia kwa kasi katika tasnia ya muziki nchini Kenya, Charisma, amepinga vikali madai yaliyosambaa mtandaoni hivi karibuni yakidai kwamba muziki wa Tanzania una ubora zaidi kuliko wa Kenya. Akijibu moja kwa moja shabiki aliyeibua mjadala huo, Charisma amesema suala la ubora wa muziki halipimwi na nchi, bali linapimwa na ubunifu, uwekezaji, na jinsi msanii anavyoweza kuwafikia mashabiki wake. Msanii huyo, amesisitiza kuwa wasanii wa Kenya wanafanya kazi kubwa na wana mitindo ya kipekee ambayo inatambulika kimataifa. Hata hivyo amewataka mashabiki kuthamini sanaa kutoka nchi zote mbili badala ya kuanzisha migawanyiko isiyo na tija, akisisitiza kuwa ushirikiano ndio utakaoukuza muziki wa Afrika Mashariki kwa ujumla. Kauli ya Charisma imepanua mjadala kuhusu ubora wa muziki Afrika Mashariki, huku wadau wengi wakitoa maoni tofauti kuhusu ukuaji, ushawishi na mchango wa tasnia ya muziki kutoka mataifa hayo mawili.

Read More
 Charisma Afichua Kukusanya zaidi ya Bra 400 Kutoka kwa Mashabiki wa kike

Charisma Afichua Kukusanya zaidi ya Bra 400 Kutoka kwa Mashabiki wa kike

Msanii wa RnB kutoka Kenya, Charisma, amefichua tukio la aina yake kuhusu namna mashabiki wake wa kike wamekuwa wakionyesha mapenzi yao kwake wakati wa maonyesho yake ya muziki. Akizungumza katika mahojiano na Zoza Podcast, Charisma amesema hadi sasa amekusanya jumla ya bra 404 zilizotupwa jukwaani wakati akiwa kwenye perfomance Amesema kwamba hakuwahi kutarajia kuishia na idadi hiyo kubwa, lakini sasa amezizoea kama sehemu ya matukio ya burudani kwenye maonyesho yake. Msanii huyo ametania kuwa sasa ana mpango wa kupeleka mzigo wote laundry ili ziwe safi kabla ya kufikiria hatua nyingine. Hata hivyo Charisma amebainisha kwamba licha ya utani unaoendelea mitandaoni, kwake ni kumbukumbu ya namna mashabiki wanavyoipokea kazi yake.

Read More
 Charisma Anua Gari Jipya la Kifahari Kutokana Mafaniko ya Muziki

Charisma Anua Gari Jipya la Kifahari Kutokana Mafaniko ya Muziki

Mwimbaji wa Kenya Charisma ameonyesha hatua kubwa aliyofikia katika safari yake ya muziki baada ya kutambulisha Mercedes-Benz E-Class yake mpya, hatua anayosema inaakisi vilele na mabonde aliyopitia kwenye tasnia. Kupitia mitandao ya kijamii, Charisma ameshukuru mashabiki wake wote kwa kumuunga mkono, akisisitiza kuwa bila wao asingefika mahali alipo leo. Amesema safari yake ya muziki imejaa maumivu na furaha, akimaanisha kuwa ingawa amekutana na changamoto nyingi, muziki pia umemletea faraja na mafanikio makubwa. Msanii huyo amekiri kuwa muziki ndicho kitu pekee anachokifanya kwa moyo wake wote, na kwamba imekuwa safari ngumu lakini yenye thawabu. Ujio wa gari hilo la kifahari umeibua wimbi la pongezi kutoka kwa mashabiki na wasanii wenzake, wengi wakimpongeza kwa juhudi, uvumilivu na kujituma katika tasnia yenye ushindani mkali

Read More