Msanii Grace Khan Ashikiliwa Rehab Kwa Deni la Milioni 5
Msanii wa muziki kutoka Uganda Grace Khan anaripotiwa kushikiliwa kwenye kituo cha tiba ya uraibu (rehab) jijini Kampala baada ya kushindwa kulipa bili zinazodaiwa kufikia zaidi ya shilingi milioni 5 za Uganda. Kwa mujibu wa vyanzo vya karibu na familia yake, ndugu wa msanii huyo wameshindwa hadi sasa kukusanya fedha hizo, hali iliyosababisha uongozi wa kituo hicho kumzuia kuondoka au kuwa na uhuru wa kutembea nje hadi deni hilo litakapolipwa. Hali hiyo imezua wasiwasi mkubwa miongoni mwa mashabiki na wasanii wenzake, huku wito ukitolewa kwa watu wenye nia njema kujitokeza kusaidia ili msanii huyo apate uhuru wake na kuendelea na safari ya kupona. Grace Khan amekuwa akipambana na uraibu wa dawa za kulevya na pombe kwa zaidi ya miaka mitatu, akiripotiwa kuingia na kutoka mara kwa mara kwenye vituo vya tiba ya uraibu. Hata hivyo, vyanzo vya ndani vinasema kuwa kurudia matumizi ya pombe mara kwa mara kumekuwa kikwazo kikubwa katika mchakato wake wa kupona.
Read More