Iyanii Aahidi Kutoa Mapato Yake ya Muziki Kwa Wafungwa

Iyanii Aahidi Kutoa Mapato Yake ya Muziki Kwa Wafungwa

Msanii wa muziki nchini Kenya, Iyanii, amewagusa wengi baada ya kutangaza uamuzi wake wa kusaidia wafungwa kupitia mapato ya muziki wake. Kupitia podcast ya Mic Check, Iyanii amesema ameahidi kutenga asilimia 20 ya mapato yote atakayopata kutokana na muziki wake ili kuwasaidia watu walioko magerezani. Msanii huyo amesema hatua hiyo inalenga kuwapa wafungwa matumaini na kuwasaidia kuboresha maisha yao wakiwa kifungoni, akisisitiza kuwa kila mtu anastahili nafasi ya pili maishani. Iyanii ameendelea kusisitiza kuwa muziki kwake si burudani pekee, bali ni njia ya kurudisha kwa jamii na kugusa maisha ya watu wanaohitaji msaada.

Read More
 Iyanii Ashinda Tuzo Mbili Kubwa

Iyanii Ashinda Tuzo Mbili Kubwa

Msanii nyota wa Afropop, Iyanii, ameendelea kung’ara kwenye tasnia ya muziki baada ya kushinda tuzo mbili katika hafla ya utoaji tuzo za Jamhuri mwaka huu Jijini Nairobi. Iyanii ametia kibindoni tuzo ya Best Male Artist of the Year, kutokana na mchango wake mkubwa na kazi zilizotamba nchini Kenya. Lakini pia ameshinda tuzo ya Music Collaboration of the Year kupitia single yake Donjo Maber, kazi iliyopokelewa kwa ukubwa na mashabiki. Kupitia Instastory yake, Iyanii amewashukuru mashabiki wake kwa kuamini safari yake ya muziki na kueleza kuwa ushindi huo ni hatua nyingine muhimu katika historia yao ya pamoja. Iyanii ambaye kwa muda amekuwa na njaa ya mafanikio, ameongeza kuwa kilicho mbele sasa ni malengo makubwa zaidi, ikiwemo kutazamia tuzo za kimataifa kama Grammy. Ushindi huu unathibitisha nafasi ya Iyanii kama mmoja wa wasanii wanaoendelea kuipa sura mpya muziki wa kizazi kipya nchini Kenya

Read More
 Msanii Iyanii Atoa Vifaa vya Muziki kwa Wafungwa Gerezani

Msanii Iyanii Atoa Vifaa vya Muziki kwa Wafungwa Gerezani

Msanii wa muziki nchini Kenya, Iyanii, ameonyesha moyo wa kutoa na kuunga mkono jamii baada ya kutembelea Gereza la Kamiti Medium kwa shughuli za Utoaji Huduma kwa Jamii (CSR). Katika ziara hiyo, msanii huyo ametoa seti kamili ya vifaa vya muziki (sound system) kwa madhumuni ya kusaidia na kukuza vipaji vya wafungwa. Msaada huo unatarajiwa kuboresha mazingira ya mafunzo ya muziki gerezani, na kutoa fursa kwa wafungwa kuendeleza talanta zao wanapohudumia vifungo vyao. Vifaa hivyo vitatumika kwenye shughuli za burudani, maonyesho ya ndani ya gereza na mafunzo ya uanamitindo wa sauti. Hatua ya Iyanii imepongezwa na uongozi wa gereza pamoja na mashabiki wake, wakisema kwamba mchango wake utawasaidia wafungwa kujenga ujuzi, kujiamini na kupata nafasi mpya za kujifunza kupitia sanaa. Ziara hiyo imeweka msanii huyo kwenye orodha ya wasanii wanaotumia sanaa na hadhi yao kuinua jamii na kuleta matumaini mahali ambapo wengi husahauliwa.

Read More