Juma Lokole Amlalamikia Wema Sepetu kwa Kukimbia Dili la Kazi
Mdau wa masuala ya burudani, Juma Lokole, ameonyesha maumivu na masikitiko makubwa kufuatia kitendo cha muigizaji maarufu Wema Sepetu kudaiwa kukimbia kazi waliyokuwa wamekubaliana. Akizungumza kwa uchungu, Juma amesema alimpa Wema dili la kazi baada ya makubaliano yote kukamilika ikiwemo kukubali kiwango cha malipo na kukatiwa tiketi ya ndege kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo. Hata hivyo, anadai kuwa muigizaji huyo aliingia mitini dakika za mwisho bila kutoa maelezo yoyote ya kuridhisha. Kwa mujibu wa Juma, kilichomuudhi zaidi ni taarifa kwamba Wema alichagua kuthamini masuala ya mapenzi kuliko kazi, jambo alilodai ni kukosa weledi na kujituma kazini. Anasema alimheshimu Wema kama msanii mkubwa, jambo lililomfanya kumpa imani kubwa, lakini matokeo yakawa tofauti na matarajio yake.
Read More