Kush Tracy: Nilitumia Pombe na Mihadarati Wiki Nzima

Kush Tracy: Nilitumia Pombe na Mihadarati Wiki Nzima

Msanii aliyeacha muziki wa kidunia na kugeukia Injili, Kush Tracy, amefunguka kuhusu maisha yake ya nyuma akieleza kuwa aliwahi kuishi kwenye uraibu wa pombe na matumizi ya mihadarati kwa kipindi kirefu kabla ya kubadili mwelekeo wa maisha na kuokoka. Kupitia podcast ya Mwakideu Live, Kush Tracy amesema kulikuwa na kipindi ambacho aliweza kunywa pombe na kutumia mihadarati kwa wiki nzima bila kupumzika, hali aliyosema ilimharibu kimwili na kiakili. Msanii huyo amesema wakati huo hakuwa na hofu wala malengo ya maisha, akifanya mambo bila kujali athari zake. Ametoa mfano wa jinsi uraibu huo ulivyomfanya kushiriki mapenzi kiholela akiwa mlevi kupindukia. Msanii huyo ameongeza kuwa safari ya kuokoka haikuwa rahisi, lakini ilikuwa uamuzi muhimu uliobadili maisha yake kabisa. Kush Tracy sasa anatumia ushuhuda wake kuwahimiza vijana kuepuka matumizi ya dawa za kulevya na pombe kupita kiasi, akisisitiza kuwa mabadiliko yanawezekana kwa yeyote anayeamua.

Read More
 Msanii Kush Tracey Aadhimisha Miaka 3 ya Kuacha Pombe na Dawa za Kulevya

Msanii Kush Tracey Aadhimisha Miaka 3 ya Kuacha Pombe na Dawa za Kulevya

Msanii wa muziki kutoka Kenya, Kush Tracey, amesherehekea kutimiza miaka mitatu bila kutumia pombe wala dawa za kulevya, akifichua kuwa safari yake ilichochewa na uamuzi wake wa kugeukia dini. Kupitia ujumbe alioweka kwenye mitandao ya kijamii, Kush Tracey amesema kuwa siku ya leo miaka mitatu iliyopita alichukua uamuzi wa kutotumia kabisa pombe, sigara, vapes/sheesha, bangi, miraa (khat), vidonge mbalimbali, ecstasy/molly pamoja na kuber. Msanii huyo ambaye aliacha muziki wa kidunia na kugeukia muziki wa injili, amekiri kuwa haikuwa safari rahisi, lakini imani na maombi vilimpa nguvu ya kuvuka kipindi kigumu cha uraibu wa dawa za kulevya. Kwa hatua hiyo, Kush Tracey anaungana na orodha ya wasanii wanaotumia majukwaa yao kuhamasisha maisha yenye afya, matumaini na mabadiliko, akithibitisha kuwa kuanza upya kunawezekana kwa yeyote aliye tayari kuchukua hatua.

Read More