Pacha wa Lil Wayne Awaomba Watanzania Wampe Sapoti Kwenye Kazi zake
Pacha wa Lil Wayne ameomba Watanzania kumuunga mkono katika kazi zake za content creation badala ya kumkatisha tamaa. Akizungumza na EATV, Wayne wa bei ya jioni amesema amekuwa akipokea kauli nyingi kutoka kwa baadhi ya Watanzania wakimtaka aache kufanya content creation na aende kulima, kauli ambazo amesema zinamuumiza sana. Ameeleza kuwa anatokea maeneo ya mijini ambayo hayana mashamba, hivyo ushauri huo hauendani na mazingira yake wala uhalisia wa maisha yake. Kijana huyo amesisitiza kuwa anachofanya si mzaha bali ni kazi halali inayompatia kipato, na akaomba jamii imuone kama kijana anayejitahidi kujitafutia maisha kwa njia ya ubunifu. Lil Wayne wa mchongo ametambulika zaidi kwa kujifananisha na rapa wa Marekani, Lil Wayne, kwa muonekano wake, mtindo wa mavazi pamoja na michoro ya tatoo mwilini. Kufanana huko ndiko kulikompa jina la Pacha wa Lil Wayne na kumfanya avutie macho ya wengi mitandaoni.
Read More