Matumizi ya Bangi Yamponza Mrembo wa Kenya
Influencer kutoka Kenya, Naomi Kuria, amefichua kuwa matumizi ya bangi yalimsababishia hasara kubwa baada ya kupoteza dili la ushawishi (influencing deal) lenye thamani ya shilingi 600,000 za Kenya. Akipiga stori na Oga Obinna, Naomi amesema kuacha kutumia bangi halikuwa jambo rahisi, huku akikiri kuwa matumizi hayo yalimuathiri kwa kiwango kikubwa katika maisha yake ya kila siku na kazi. Ameeleza kuwa bangi ilimfanya kuwa mvivu kupita kiasi, kukosa motisha ya kufanya kazi na kutumia muda mwingi akiwa amejilaza kwenye sofa bila kufanya jambo la maana. Kwa mujibu wa Naomi, kampuni aliyokuwa akifanya nayo kazi ilimtaka kurekodi upya video ya matangazo, lakini alishindwa kutimiza agizo hilo kwa wakati kutokana na uvivu uliotokana na matumizi ya bangi. Hatimaye, brand hiyo iliamua kusitisha mkataba wake, jambo lililomgharimu dili hilo nono. Mrembo huyo, amesema kuwa bangi pia ilimuathiri kiakili, hasa kwenye kumbukumbu na mawasiliano. Amesema alikuwa akisahau maneno ya Kiingereza na kushindwa kujieleza kwa ufasaha, hali iliyomletea changamoto kubwa katika kazi yake ya uinfluencer.
Read More