PALASSO AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA ROGER LUBEGA

PALASSO AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA ROGER LUBEGA

Msanii nyota kutoka Uganda Pallaso amefunguka uhusiano wake na meneja wa Spice Diana, Roger Lubega. Katika mahojiano yake hivi karibuni Pallaso amesema kwa miaka ambayo amefanya kazi na Roger Lubega amekuwa mtu mwema, kwani amekuwa mstari wa mbele kupigania tasnia ya muziki nchini uganda. Kauli ya Gravitty omutujju imekuja siku chache baada ya Gravity Omutujju kumshambulia Roger Lubega kwa madai ya kuwa mbinafsi na mnafiki kwenye kazi za za muziki. Utakumbuka mwaka wa 2016 Pallaso alimpa kazi Roger Lubega kuwa meneja wake baada ya kuacha kufanya kazi na Ziza Bafana

Read More
 PALASSO AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA, TEAM NO SLEEP

PALASSO AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA, TEAM NO SLEEP

Mwanamuziki kutoka uganda Palasso amemtambulisha msanii wake mpya kwenye lebo yake ya muziki ya Team No Sleep. Kupitia ukurasa wake wa Twitter  amesema msanii wake anaitwa Carolina huku akimwagia sifa kwamba ana kipaji cha kipekee, hivyo ana Imani kuwa ataipeleka lebo yake kwenye ngazi ya kimataifa.. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” amesema Carolina atakuwa chini ya lebo ya team no sleep ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki ambapo amewataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo kwenye tasnia ya muziki nchini lakini pia wakae mkao wa kula kupokea nyimbo zake “Karibu msanii kama wewe, mwenye kipaji, mrembo, Kijana na aliyejaa nguvu ni mali kwa kampuni kama yetu. Carolina sasa amesainiwa rasmi na Kampuni ya Team Good Music, Hongera. Hatuwezi kusubiri kuanza kufanya kazi na wewe. ,” Pallaso alitweet. Kusainiwa kwa Carolina kunakuja miaka kadhaa baada ya msanii Jowy Landa kuigura lebo ya Team Good Music kwa njia tatanishi. Utakumbuka mapema mwaka huu Palasso aliahidi kuwasaidia vijana wanaochipukia kwenye muziki nchini Uganda kwa kuanza kuwasaini ndani ya lebo  yake ya muziki.

Read More
 PALASSO ATANGAZA KUJA NA ONESHO LAKE MWEZI JULAI MWAKA HUU

PALASSO ATANGAZA KUJA NA ONESHO LAKE MWEZI JULAI MWAKA HUU

Msanii nyota nchini Uganda pallaso ametangaza ujio wa   onesho lake la siku mbili litakalofanyika katika ukumbi wa Lugogo Cricket Oval. Kupitia ukurasa wake wa Twitter Pallaso pamoja na uongozi wake wamesema onesho hilo litafanyika tarehe 1 na 2 mwezi julai mwaka wa 2022. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Malamu” ametoa rai kwa mashabiki zake kumuonyesha upendo na kumuunga mkono katika onesho lake hilo kwani hataki kutumbuiza kwenye ukumbi ambao hawana watu. Cricket Oval ni ukumbi mkubwa maarufu uliopo jijini kampala wenye kuingiza idadi ya watu elfu 20 ambao unatumiwa na mastaa wakubwa duniani kufanya show zao. Utakumbuka Pallaso kwa sasa anaendelea na Golden tour, ziara ya mwezi moja ambayo inalenga kuzunguka kwenye miji zaidi ya 25 nchini uganda ikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu wa Machi.

Read More
 PALASSO KUANZA GOLDEN TOUR NCHINI UGANDA MACHI 6 2022

PALASSO KUANZA GOLDEN TOUR NCHINI UGANDA MACHI 6 2022

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Palasso anatarajia kuaza tour yake nchini humo ambayo itakuwa na show 25 kwa kipindi cha mwezi mmoja. Kupitia ukurasa wake rasmi wa instagram Palasso, ameipa ziara hiyo jina la Golden Tour  na itaanza machi 6  hadi machi 31 mwaka wa 2022. Ziara hiyo inatarajiwa kuzunguka kwenye miji mbalimbali nchini Uganda ikiwemo Lukaya, Katosi, Soroti, Kasanda na nyingine. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Maluma” amesema lengo la kuja na Golden tour ni kwa ajili ya kuwashukuru mashabiki zake ambao wamekuwa wakimsapoti tangu aanze safari ya muziki wake.

Read More