Pritty Vishy Atishia Kumshushia Stevo Simple Kipigo cha Mwaka

Pritty Vishy Atishia Kumshushia Stevo Simple Kipigo cha Mwaka

Mrembo wa mitandaoni Pritty Vishy ametishia kumshushia kipigo cha mwaka msanii Stevo Simple Boy baada ya kukasirishwa na madai yaliyoibuliwa na msanii huyo kuwa amefanya upasuaji wa kuongeza makalio (BBL). Katika ujumbe wake Instastory, Pritty amewataka mashabiki wasimlaumu endapo atachukua hatua ya kumuadhibu Stevo Simple Boy, akisisitiza kuwa amechoshwa na tuhuma zinazomhusisha na masuala ya mwili wake. Kupitia kauli zake kwa mashabiki, Pritty Vishy amekanushai madai ya kufanyiwa BBL akionyesha kukerwa na kile alichokitaja kama kuchafuliwa jina na kudhalilishwa hadharani. Mrembo huyo, ameonya kuwa hatavumilia kusemwa vibaya. Kauli ya Pritty Vishy imekuja baada ya Stevo kudai kuwa hawezi kumrudia mrembo huyo kimapenzi kutokana na uamuzi wake wa kufanya BBL. Alienda mbali zaidi na kusema kuwa anapendelea wanawake wenye maumbo ya asili kuliko wanaotumia madawa kubadilisha miili yao.

Read More