Msanii wa Bongo Fleva Shetta Ameteuliwa Kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva Shetta Ameteuliwa Kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam

Msanii wa Bongo Fleva na Diwani wa Kata ya Mchikichini, Ilala, Nurdin Juma, maarufu kama Shetta, amechaguliwa kuwa Meya wa Jiji la Dar es Salaam baada ya kushinda kwa kura nyingi katika uchaguzi uliofanyika jana, Desemba 4, mwaka 2025. Katika uchaguzi huo uliohusisha wajumbe 51, Shetta alipata kura 48, huku kura mbili zikipigwa kupinga utenzi wake. Hatua hii inamuweka rasmi katika nafasi ya juu ya uongozi wa jiji, akichukua nafasi ya Omary Kumbilamoto, aliyemaliza muhula wake baada ya kushikilia wadhfa huo kati ya mwaka 2021 – 2025. Sambamba na uchaguzi huo, John Mrema amechaguliwa kuwa Naibu Meya wa Jiji la Dar es Salaam, akipata kura 49, ishara ya uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wajumbe wa baraza. Uteuzi wa Shetta umeibua pongezi kutoka kwa wadau wa sanaa, wananchi na viongozi mbalimbali, huku wengi wakitaja hatua hiyo kama ishara ya kupanuka kwa ushiriki wa wasanii katika masuala ya uongozi wa jamii.

Read More