Sho Madjozi Aeleza Wasiwasi Kuhusu Hali Tanzania

Sho Madjozi Aeleza Wasiwasi Kuhusu Hali Tanzania

Msanii nyota kutoka Afrika Kusini, Sho Madjozi, ameonyesha wasiwasi wake kuhusu hali ya mawasiliano na hali ya kisiasa nchini Tanzania, akisema kuwa tangu jana hajafanikiwa kuwasiliana na marafiki zake walioko nchini humo. Sho Madjozi amesema kuwa amehisi hofu kubwa kutokana na hali ya ukosefu wa mawasiliano, huku akisisitiza upendo wake kwa Tanzania na watu wake. Amebainisha kuwa anaamini Watanzania, kama watu wengine wote, wana haki ya kuchagua viongozi wao na pia kuandamana kwa amani bila hofu wala vurugu. Msanii huyo ametoa wito kwa walioko madarakani kusikiliza sauti za wananchi, akisema kuwa dunia inafuatilia yanayoendelea nchini humo na kwamba kuzima mitandao hakutaweza kuzima tamaa ya watu kuona mabadiliko. Aidha, amewataka wale wanaoshiriki maandamano kuendeleza amani na kujiepusha na vitendo vya vurugu, akisisitiza kuwa vurugu ni silaha ya wale wanaopinga mabadiliko. Sho Madjozi amehitimisha ujumbe wake kwa maneno ya matumaini kupitia ukurasa wake wa Instagram, akisema kuwa maombi ya watu yanapaswa kujibiwa kwa mabadiliko, siyo kwa ukandamizaji, huku akisisitiza kuwa Tanzania daima itabaki kuwa nchi anayoiweka karibu na moyo wake.

Read More