Wakuu Music Atoa Onyo kwa Marapa wa Kenya kwa Kukosa Ubunifu

Wakuu Music Atoa Onyo kwa Marapa wa Kenya kwa Kukosa Ubunifu

Tasnia ya muziki wa rap nchini Kenya imewaka moto baada ya Wakuu Music kutoa onyo kali kwa wasanii Toxic Lyrikali na Breeder LW, kufuatia kuibuka kwa diss tracks nne zilizowalenga wasanii wengine kama Trio Mio na Maandy. Akiongea kwa hisia, Wakuu Music alimkosoa Toxic Lyrikali, akibainisha tofauti kubwa iliyopo kati yao. Alisisitiza kuwa yeye ni msanii aliyewekeza kikamilifu kwenye kazi yake na kutengeneza jina lake kupitia muziki, huku akimtaja Toxic kama mtu anayejenga jina lake zaidi kupitia mitandao ya kijamii. Akimgeukia Breeder LW, Wakuu Music alimtuhumu kuwa msanii anayezungumza kupita kiasi na kutafuta “kiki” kupitia mivutano ya mtandaoni. Alipuuzilia mbali madai kuwa Breeder na kundi lake wanapanga njama ya kumshambulia, akieleza kuwa hayo ni mbinu za kutafuta umaarufu wa haraka usio na msingi. Kwa upande wa Trio Mio, Wakuu Music amemtaja kama kijana ambaye hawafikia kwenye kiwango cha kumkabili, akieleza kuwa mawasiliano yao ya awali hayakuzaa matokeo yoyote na kwamba Trio hapaswi kuvutwa kwenye drama anazodai kusukwa na Breeder. Maandy pia aliingia kwenye orodha ya walioshambuliwa, ambapo Wakuu Music alidai kuwa msanii huyo alijaribu kutumia mahusiano ya kimapenzi na Breeder LW kama njia ya kupata umaarufu. Alisisitiza kwamba mvutano huu haupaswi kuwa tiketi ya Maandy kujipandisha kimuziki. Wakuu Music pia aligusia kwamba masuala yoyote yanayomhusu Octopizzo yanaweza kushughulikiwa kiutulivu bila drama za mitandaoni. Hata hivyo, alituma onyo kali kwa yeyote anayefikiria kumjibu, akisema kuwa akipata majibu kutoka kwao ataweka wazi tabia zao mtandaoni na hivyo kusisitiza wasijaribu kujibizana naye. Sakata hilo limezidi kuchochea mjadala mitandaoni, huku mashabiki wakisubiri kuona iwapo wasanii waliolengwa watatoa majibu yao au kama mvutano huu wa rap utaendelea kupamba moto.

Read More
 Wakuu Music  Aachia Diss track ya Pili Baada ya Toxic Lyrikali Kuidharau ya Kwanza

Wakuu Music Aachia Diss track ya Pili Baada ya Toxic Lyrikali Kuidharau ya Kwanza

Bifu kati ya Wakuu Music, na rapa Toxic, limechukua sura mpya baada ya Wakuu kuachia diss track yao ya pili iitwayo “Coffin,” ambayo inamlenga moja kwa moja msanii Toxic Lyrikali. Hii inakuja siku chache tu baada ya Toxic Lyrikali kupuzilia mbali diss track ya kwanza kwa kuita mchongoana ambapo alienda mbali zaidi na kusema kwamba hana muda wa kujibizana na wasanii wanaotafuta umaarufu kupitia mafanikio yake ya muziki. Katika diss track ya “Coffin,” Wakuu Music amejibu kwa toni kali zaidi, akichana kwa maneno makali na mafumbo yanayoashiria kuongezeka kwa mvutano kati yao na mpinzani wao. Diss track hiyo imeibua hisia kali mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakisifu ubunifu na uchezaji wa maneno, huku wengine wakisema bifu hiyo inazidi kupandisha joto la ushindani katika muziki wa Hiphop. Mashabiki sasa wanasubiri kuona kama Toxic Lyrikali atajibu au ataendelea kupuuzia kama alivyofanya kwa diss track ya kwanza.

Read More