Sports news

Tanzania Yaaga Mashindano ya CHAN Baada ya Kichapo Kutoka kwa Morocco

Tanzania Yaaga Mashindano ya CHAN Baada ya Kichapo Kutoka kwa Morocco

Tanzania imebanduliwa rasmi katika mashindano ya soka ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN), baada ya kuchapwa bao 1-0 na Morocco katika robo fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Katika mechi hiyo ya kusisimua lakini yenye presha kubwa kwa wenyeji, kipindi cha kwanza kilimalizika bila timu yoyote kuona lango. Hata hivyo, Morocco mabingwa mara mbili wa CHAN mwaka 2018 na 2020 walionyesha uhodari wao katika kipindi cha pili na kufunga bao la pekee la ushindi katika dakika ya 65 kupitia kwa mshambulizi wao mahiri, Oussamma Lamloui. Bao hilo lilimfanya kuwa kinara wa mabao kwenye mashindano haya, akiwa amefunga jumla ya mabao manne hadi sasa.

Licha ya juhudi za Taifa Stars kutafuta bao la kusawazisha, mashambulizi yao yalizimwa na safu imara ya ulinzi ya Morocco pamoja na kipa wao aliyekuwa makini muda wote wa mchezo.

Kwa matokeo haya, Tanzania imekuwa taifa la pili mwenyeji kuaga mashindano kabla ya hatua ya nusu fainali, ikifuatia Kenya ambayo iliondolewa na Madagascar kwa mikwaju ya penalti 4-2 baada ya sare ya bila kufungana katika muda wa kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *