Entertainment

Terence Creative Aahidi Msaada wa Kifedha kwa Shalkido Baada ya Kumtusi

Terence Creative Aahidi Msaada wa Kifedha kwa Shalkido Baada ya Kumtusi

Mchekeshaji maarufu Terence Creative ametoa majibu ya busara baada ya kutukanwa na msanii wa Gengetone, Shalkido, kupitia mitandao ya kijamii.

Katika ujumbe wake, Terence amemshauri Shalkido kuangalia upya mtazamo wake wa maisha, akisisitiza kuwa namna mtu anavyojipanga kimaisha ndiyo huunda tabia yake, na hatimaye huathiri mustakabali wake. Amemkumbusha kuwa makosa ya zamani hayapaswi kumzuia kusonga mbele, akimtakia heri na baraka katika safari yake ya maisha.

Mbali na ushauri huo, Terence ameahidi kumpa Shalkido msaada wa kifedha wa shilingi elfu ishirini pindi atakaporejea nchini, akisisitiza kuwa nia yake ni kumsaidia kuanza upya. Hatua hiyo imepongezwa na mashabiki wengi waliomtaja kama mfano wa hekima na ukarimu licha ya kuchokozwa.

Mzozo kati ya Shalkido na Terrence ulitokea baada ya Terence kuwashauri wasanii kuwekeza mapema wakiwa bado wanapata mafanikio katika muziki, jambo ambalo halikumpendeza Shalkido. Shalkido alijibu kwa hasira akimtusi Terence na kudai kuwa anatumia changamoto zake za kuomba msaada kama njia ya kutengeneza maudhui.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *