
Timu ya mchezo wa hockey ya wanawake ya USIU yatoka sare na Platau Queens ya Nigeria kwenye mashindano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Afrika
Timu ya mchezo wa hockey ya wanawake ya USAU ilitoka sare na Platau Queens ya Nigeria kwa kufungana bao moja kwa moja kwenye mashindano ya kuwania kombe la klabu bingwa barani Afrika mjini Ismailia Misri. Timu hiyo sasa ina alama saba kundini B, alama mbili nyuma ya Sha ya Misri.
Kwenye mechi nyingine Western Jaguar ilijipatia ushindi wao wa kwanza kabisa kwenye mashindano hayo kwa kuitandika ni J Flickers kwa mabao sita kwa moja ushindi huo hata hivyo hautatosha kuifuzisha timu hiyo kwa mechi za fainali hasa baada ya kupoteza mechi tatu za awali za makundi.
Kwenye mechi nyingine Mombasa sports club ilishinda Sha klabu ya Misri bao moja kwa sifuri kwenye mechi ya wanawake. Timu hiyo sasa imejipatia jumla ya alama saba baada ya kuishinda mechi moja ya awali ya makundi . Shark sports club ya Misri ilishinda Kada stars ya Nigeria kwa magoli matatu kwa moja kwenye mechi ya wanaume.
Timu zitakazomaliza katika nafasi za kwanza katika kila kikundi zitafuzu kwa fainali ilhali zile zitakazomaliza ya pili zitashiriki katika mechi za kung’ang’ania nafasi ya tatu na nne. Mashindano hayo yaliyoshirikisha timu kumi za wanawake na kumi za wanaume zitakamilika ijumaa hii.