Entertainment

TREVOR NOAH AKANUSHA MADAI YA KUMCHOMEA KANYE WEST, KUONDOLEWA KWENYE GRAMMY

TREVOR NOAH AKANUSHA MADAI YA KUMCHOMEA KANYE WEST, KUONDOLEWA KWENYE GRAMMY

Mchekeshaji wa Afrika Kusini Trevor Noah amefunguka baada ya kuhusishwa na taarifa za Kanye West kuondolewa kwenye orodha ya watumbuizaji wa Tuzo za Grammy.

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa twitter, Trevor Noah ameandika ujumbe unaosomeka “I said counsel Kanye not cancel Kanye.” akimaanisha alitaka YE apatiwe msaada wa kiushauri na sio kumuondoa kwenye show ya Grammy.

Trevor ambaye atakuwa mshereheshaji wa Tuzo za Grammy mwaka huu, alihusishwa na kitendo cha kumchoma Kanye West hadi kuondolewa kwenye list ya watumbuizaji wa tuxo hizo kufuatia majibizano yao mitandaoni ambayo yalipelekea YE kumtolea Trevor Noah kauli za kibaguzi baada ya kuandika kitu kuhusu Kim Kardashian.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *