
Staa wa muziki kutoka marekani Tyga amefunguliwa mashtaka kwa kumpiga mpenzi wake wa zamani Camaryn Swanson.
Kwa mujibu wa tovuti ya TMZ, mrembo huyo alifika nyumbani kwa Tyga mishale ya saa 9 usiku Jumatatu wiki ambapo awali aliambiwa asifike nyumbani hapo.
Taarifa zinaeleza kwamba Camaryn alikuwa amelewa, lakini Tyga alimruhusu aingie ndani kwa ajili ya kuzungumza naye.
Baadaye zilianza kusikika kelele za Camaryn ambaye ameiambia polisi kwamba Tyga alikuwa akimrushia ngumi wakati wa majibizano yao.
Mama yake mzazi alifika na kumchukua kisha kuwapigia simu polisi kutoa taarifa.
Polisi walifika nyumbani kwa Tyga siku hiyo hiyo kwa ajili ya uchunguzi na Tyga ameripotiwa kuandikisha kutoa maelezo kwa upande wake ikiwa tayari amefunguliwa kesi ya unyanyasaji wa nyumbani.
Camaryn ame-share picha zake za majeraha baada ya tukio hilo.