Entertainment

Rapa Tyga akanusha vikali kuwa penzini na Alabama

Rapa Tyga akanusha vikali kuwa penzini na Alabama

Rapa kutoka nchini Marekani Tyga amekanusha uvumi kwamba alifanya mapenzi na binti wa Travis Barker, Alabama Barker kwa kusema kwamba uvumi wa ujauzito ulioanzishwa na rapa Bhad Bhabie ni ujinga mkubwa zaidi aliowahi kusikia.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa X amepuzilia mbali madai hayo kwa kusema kuwa hajawahi kuwa na mahusiano na binti huyo.

Wakati huo huo Alabama pia kupitia ukurasa wa Instagram amekanusha vikali madai ya kuwahi kuwa na ujauzito na kisha akautoa. Mrembo huyo amesisitiza kuwa hajawahi kuwa kwenye mahusiano na Tyga Wala Soulja Boy kama jinsi walimwengu wanavyodai mtandaoni.

Kauli ya wawili hao imekuja siku chache baada ya rapa Tyga kudaiwa kuwa alifanya ngono na binti wa Travis Barker mwenye umri wa miaka 19,Alabama Barker.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *