
Sosholaiti maarufu wa Kenya, Vera Sidika, amewakata kalima wakosoaji wake wanahoji uhalali wa gari lake aina Range Rover baada ya kushiriki video ya safari yake jijini London, Uingereza, ambako alinunua gari jipya la kifahari.
Vera alionekana akipokea gari hilo kwenye duka la magari na baadaye kushiriki matukio ya furaha yake kupitia reel alizopakia kwenye mitandao ya kijamii. Hata hivyo, baada ya baadhi ya wakosoaji kudai kuwa gari hilo halikuwa mali yake, aliamua kufunga mjadala kwa kuonyesha logbook rasmi kuthibitisha umiliki wake.
Pamoja na uthibitisho huo, Vera hakusita kuwatolea uvivu wakosoaji hao, akiwashutumu kwa kueneza habari za kupotosha. Mrembo huyo ameenda mbali za kumeweka wazi kuwa yeye si staa wa kawaida anayepaswa kudharauliwa, akisisitiza kuwa kiwango chake cha maisha kiko juu mno ikilinganishwa na mtazamo wa waliomkosoa.
Haikuishi hapo, alijitapa kwa maneno makali akidai ana uwezo mkubwa wa kifedha kiasi kwamba akikasirishwa, anaweza hata kuwanunulia baadhi ya wanablogu wanaomzungumzia vibaya magari ili kuwaondoa kwenye kile alichokiita fikra za kimaskini.