
Staa wa muziki kutoka Uganda Vinka amekiri kwamba aliogopa kusaini mkataba na lebo ya muziki ya Sony music, alipotafutwa na lebo hiyo kubwa duniani.
Hitmaker huyo “Thank God” amesema alikuwa ameridhishwa na utendakazi wa usimamizi wake wa Swangz Avenue, hivyo hakuona umuhimu wa kufanya kazi na lebo nyingine ya muziki.
Vinka amesema kwa sasa anafurahia maisha yake ndani ya lebo ya Sony kwani inafanya kazi nzuri katika usambaza muziki wake, hivyo hajutii kutia mkataba na lebo hiyo ya kimataifa.
Hata hivyo Vinka amesema licha ya kufanya kazi na sony,bado lebo yake ya zamani ya Swangz avenue inasimamia shughuli ya wanaotaka atumbuize kwenye matamasha ya muziki.