
Mtunzi wa nyimbo Black Skin alipelekwa katika gereza la Kitaalya Alhamisi wiki iliyopita kwa mashtaka ya kumlaghai bosi wa Gagamel, Bebe Cool.
Wasanii kadhaa nchini Uganda wamejitokeza na kumtaka Bebe Cool amsamehe msanii huyo kwani wanaweza kutatua tofauti zao bila kuhusisha vyombo vya usalama.
Mwanamuziki Vampino, ambaye ni rafiki wa karibu wa Black Skin ametoa wito kwa Bebe Cool aache suala hilo kwa manufaa ya tasnia ya muziki nchini Uganda.
“Sanaa siku zote ni zawadi, tulitatue hili na tuwe na maelewano katika tasnia yetu ya ubunifu, jela sio suluhisho pekee,” Vampino aliandika kwenye kurusa zake kwenye mitandao ya kijamii.
Wasanii wengine ambao wamemtaka Bebe Cool amuachilie huru wa blacksini ni pamoja na; prodyuza Eno Beats, Kalifah Aganaga, Pallaso na wengine wengi.
Purukushani kati ya Bebe Cool na Black Skin ilianza pale mwandishi huyo wa nyimbo alipotumia mitandao ya kijamii kumtuhumu Bebe Cool kuwa ameshindwa kulipa deni lake la shillingi elfu 15 za Kenya baada ya kumuandikia wimbo uitwao, “Gyenvude”.
Haikuishi hapo alienda mbali zaidi na kusema kuachia toleo lake la wimbo wa “Gyenvude”, jambo lilimkasirisha Bebe Cool kwani Black Skin pia aliapa kumumaliza Bebe Cool kimuziki.