
DJ mkongwe nchini DJ Pinye amejipata pabaya mara ya baada ya wasanii wa muziki nchini kumsuta vikali kwa kauli yake aliyotoa majuzi kuwa ni vigumu kupiga muziki wa Kenya ughaibuini kutokana na muziki huo kukosa ubora ambao unahitajika kimataifa.
Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa Nairobi Gossip Club wasanii wa Kenya wakiongozwa na Kenrazy wameokana kukasirishwa na kauli hiyo ya DJ Pinye ambapo wamemtaka DJ huyo akome kuwavunjia heshima wa wasanii wa kenya heshima kwa lengo la kujitakia makuu.
Kauli ya Kenrazy imetiwa uzito na VDJ Jones pamoja Bien wa Sauti Sol ambao wamesema DJ Pinye muda wake umepita na hana usemi keny muziki wa Kenya kwani ameishiwa na mawazo ya kufanya kazi yake ya kudeejay ndio maana amehamua kuwaingilia wanamuziki wa kenya ambao wanatia bidii kwenye kazi zao.
Ikumbukwe juzi kati DJ Pinye kwenye mahojiano na Standard aliwapa wasanii wa Kenya changamoto kutoa nyimbo zenye ubora ambazo zitapigwa katika mataifa kama Nigeria, Afrika Kusini na mataifa mengine ambayo yanaongoza kimuziki duniani.