
Aliyekuwa msanii wa EMB Weezdom amevunja ukimya wake baada ya Willy Paul kumtaja akijijitea kuhusu tuhuma za kumbaka Diana Marua.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Weezdom amesema watajaribu kumpatanisha willy paul na bahati faraghani kupitia marafiki na wanafamilia kabla hajatoa upande wake wa stori.
“Hallo Fam I’m aware that nimetajwa Sana by Pozze about whatever that is going on ..Amidst all the allegations za hii story ya Diana…Bahati na Willy Paul are True Brothers and both are my friends we’ll try to see if we can settle this privately through Friends and Family. Ikishindikana, the truth shall set the innocent free,” aliandika Weezdom kupitia ukurasa wake wa Instagram.
Kauli ya Weezdom inakuja mara baada ya Willy Paul kumtaja kama shahidi ambaye atamsaidia kushinda kesi dhidi Diana Marua ambaye alidai bosi huyo wa Saldido alimrubuni na kisha akajaribu kumbaka